“TUCHANGAMKIE FURSA YA MIKOPO ISIYO NA RIBA”DENDEGO - MTWARA MIKINDANI MANISPAA

Jumatatu, 17 Julai 2017

“TUCHANGAMKIE FURSA YA MIKOPO ISIYO NA RIBA”DENDEGO

Wananchi  Wa Mtwara wametakiwa kuchangamkia fursa ya kupata mikopo, isiyo na riba kwenye benki ya watu wa Zanzibar (PBZ),ambayo imefungua matawi mawili Mkoani Mtwara kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki.
Hayo yamesemwa  na Mh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kwenye sherehe za ufunguzi wa matawi 2 ya benki  hiyo, zilizofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Posta Mjini Mtwara Tarehe 17 Juni 2017.
Dendego alisema kuwa, uwepo wa benki hiyo utasaidia kuinua kipato cha Wananchi wa Mtwara hasa wafanya biashara wadogo wadogo, kwa kuwa  benki hiyo imelenga utoaji wa mikopo isiyo na riba. Kwa  kuwa wafanya biashara wengi wanaumizwa na riba kubwa.
Pia amewahakikishia benki ya watu wa Zanziba kuwa atawaunganisha na  Wafanyabiashara ili waweze kuchukua mkopo katika benki hiyo, ili waweze kufungua viwanda na baadae waweze kuchangia pato la Taifa.
Pamoja na hayo Dendego amepongeza hatua ya PBZ  kuweka matawi Tanzania bara, kwani ni ishara tosha ya kuonesha uhusiano uliopo umeimarika, na kwamba sehemu yoyote mtu anaweza kuishi kwani hayo ni matunda ya Muungano.
Aidha alimalizia hotuba yake kwa kuwataka Wafanya biashara kutafuta fedhakwa njia ya halali na kuahidi kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa atasimama imara kuitangaza benki ya watu wa Zanziba kwa kuwa inafanya mambo mazuri ikiwemo Uhamasishaji wa zoezi la usafi kila mwezi MkoaniMtwara.
Awali akisoma Taarifa ya benki hiyo Mkurugenzi Mtendaj, Alisema benki ya watu wa Zanziba ilianza na mtaji wa Tsh. 16milioni mwaka 1996  hadi kufikia bilioni 57 kwa sasa.  Na kwamba fedha hizo zitasaidia kutoa huduma mbali kwa wana Mtwara ikiwemo kutoa mikopo stahiki, Kuhamasisha wafanyabiashara wadogowadogo waweze kuunda vikundi, Kutoa mikopo ya Elimu kwa mteja mmoja mmoja, Kutoa mikopo ya nyumba, gari kwa mteja mwenyewe.
Akisoma Taarifa kwa niaba ya wateja wengine Musa Ndazigula amewataka wateja wanaokopa katika benki hiyo kurudisha fedha kwa wakati ili watu wengine waweze kukopa. Aidha ameomba wafanyakazi wa PBZ Kuangalia na wafanya biashara wadogo wadogo kama boda boda na mama lishe na wao waweze kupewa mikopo.

Hakuna maoni:

Copyright: mtwaramikindanimc©2018